Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza  amesema sababu ya kumwita msanii Nandy ofisini kwao jana Julao 30, ni kutokana na picha alizopost kwenye mtandao wa Instagram ambapo kwa mujibu wa Basata wamesema sio picha nzuri. 


Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Godfrey Mngereza amesema kuwa wamemwita kuzungumzia kuhusu utaratibu wa picha alizopost Instagram ambazo hazikuwa nzuri. 


"Mara nyingi tumekuwa na utaratibu wa kuzungumza na wasanii, kuna picha kadhaa ambazo alikuwa amezirusha kwenye mtandao wa Instagram yake ambazo hazikuwa nzuri, kwa hiyo mahali alipofikia yeye si vizuri kupost picha kama zile,  vilevile kuwa makini na suala la mitandao hivyo ndiyo vitu tulivyomkumbusha tena kwa njia chanya kabisa, sisi kama Basata tuna wajibu wa kuwakumbusha wasanii kabla hatujaenda kwenye upande wa adhabu" Katibu Mtendaji Basata Godfrey Mngereza