Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N’Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa, 29. (Gazzetta dello Sport, via Metro)

Leicester City v Chelsea FC - Premier League

 

Bosi wa Inter, Antonio Conte amekuwa akivutiwa na nyota huyo tangu alipokuwa Stamford Bridge na wawili hao waliweza kutwaa taji la Premier League wakiwa pamoja Chelsea.

Kante mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akisumbuliwa na majeraha huku mkataba wake ndani ya Chelsea ukitarajiwa kumalizika mwaka 2023.

Zenit St Petersburg wameeleza nia yao ya kumsajili beki anayekipiga katika klabu ya Liverpool Dejan Lovren, 31. (Liverpool Echo)

AC Milan wanafikiria kumnunua mashambuliaji wa Real Madrid raia wa Serbia Luca Jovic, 22, ambaye anakodolewa macho na Leicester City na Arsenal. (Calciomercato,via Leicester Mercury)Luca Jovic

Kai Havertz anataka kuondoka Bayer Leverkusen kwasababu walishindwa kufuzu katika michunao ya klabu bingwa Ulaya hivyobasi Chelsea watalazimika kuhakikisha wanafuzu katika michuano hiyo ili kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumain 21 kujiunga na timu hiyo.. (Bild)

Bayern Munich wana mpango wa kuwanasa viungo wawili wanaocheza ligi kuu ya Ufaransa, Tonguy Ndombele wa Tottenham, 23, na Tiemoue Bakayoko. (Le 10Sport)

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 38, amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wake ndani ya AC Milan kwa kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliofanyika kuhusu mkataba ikiwa sasa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kufikia ukingoni. (Sky Sports)Tonguy Ndombele

Mashabiki 5,000 waliruhusiwa kuingia uwanjani kutazama mechi ya kirafiki ya Paris St Germain, mechi iliyoitoa kifua mbele kwa 9-0 dhidi ya wenyeji Le Havre. (France 24)

The post N’Golo Kante kutimka Chelsea, Conte amsubiri kwa hamu Inter appeared first on Bongo5.com.