Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania Emmanuel Mbasha amonyesha nia ya kuutaka Ubunge baada ya leo hii kuchukua fomu ya kugombea katika Jimbo la Iramba Mashariki Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida.

Kutoka upande wa kushoto Emmanuel Mbasha akichukua fomu ya kugombea Ubunge

Akitangaza nia hiyo kwenye picha na ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa Instagram Emmanuel Mbasha ameandika kuwa

Mungu kama uishivyo nakuomba nibariki safari yangu hii mpya ya kuwatumikia wananchi wa Mkalama, nimechukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Iramba Mashariki, Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida, naomba maombi yenu rafiki zangu wote, Mungu ibariki Tanzania

The post Naomba maombi yenu – Emmanuel Mbasha autaka Ubunge  appeared first on Bongo5.com.