Siku moja baada ya Mzee Yussuf kutangaza kurudi kwenye muziki, amewashukia wanaomnanga na kueleza anapaswa kujihurumia kurudi kwenye muziki ni yeye na sio mtu mwingine.

Mzee Yussuf ameyasema hayo Alhamisi hii Julai 23, alipokuwa akihojiwa na Dida ndani ya WafasiFm.

Itakumbukwa, Msanii huyo alitangaza kuacha kuimba taarabu mwaka 2016 na kujikita katika shughuli za ualimu wa dini.

Juzi Julai 22, 2020 aliwashtua wengi alipoweka tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza tukio la uwepo wake katika viwanja vya Dar Live sikukuu ya IDD El Haji, tukio aliloliita 'Mzee Yussuf anarudi Mjini'.

Baadhi ya watu wamekuwa na maoni tofauti, wengine wakimtukana huku wengine wakionyesha kumuhurumia kwa hatua hiyo ukizingatia alishaenda hadi kuhiji #Makka.

Akizungumza akiwa #Wasafifm, Mzee Yussuf amesema watu hawapaswi kumuhurumia, kwani anatakiwa kujihurumia mwenyewe. "Naomba watu wasiwe na jazba kuhusu maamuzi yangu, kwani kama ni kuadhibiwa nitaadhibiwa mimi”

"Isitoshe katika maamuzi haya sio kwamba nimeacha dini yangu bali nimerudi kwenye muziki hivyo waliokasirika huenda wakaja kufurahi nami siku zijazo,"amesema Mzee