Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi baada ya kuvamia Benki ya CRDB tawi la Igoma jijini Mwanza.

Jambazi huyo akiwa na wenzake walivamia benki hiyo majira ya Saa 8:00 Usiku na kukata bati la paa na dari ili kupata upenyo wa kuingia ndani kwa lengo la kutaka kuiba fedha.

Akizungumza na wandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa Mwanza ACP Muliro Jumanne amesema kundi hilo la majambazi bado idadi yao haijafahamika lakini walivamia benki hiyo na kuvunja eneo la nyuma la benki hiyo.

Licha ya wahalifu hao kuvamia benki hiyo na kuingia ndani walifanikiwa kuvuruga droo za ofisi hizo lakini hawakuweza kufanikiwa kuiba fedha zilizokuwa zimehifadhiwa sehemu maalumu.

The post Mwanza: Jambazi auawa kwa risasi baada ya kuvamia benki ya CRDB appeared first on Bongo5.com.