Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Dalali Malongo (20), mkazi wa kijiji cha Majimoto Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mume wake Kisabo Joseph, baada ya kumnyima tendo la ndoa.

Taarifa ya tukio hilo imetolewa Julai 16, 2020 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga, na kuongeza kuwa mara baada ya kutekeleza unyama huo hata yeye alijiua, ambapo mpaka sasa Polisi hawajabaini sababu hasa ya mke kumnyima tendo la ndoa mume wake.

“Katika maisha yao ya ndoa inasemekana marehemu alikuwa anahitaji kupata tendo la ndoa kutoka kwa mareehemu mke wake, lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu ambazo hazijaweza kufahamika, na ndipo alipoamua kumsindikiza kisimani na ndipo alipoamua kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni mwake”, amesema Kamanda Kuzaga.

Jeshi la polisi linatoa wito kwa wanandoa na Wananchi kwa ujumla kutojichukulia sheria mkononi, endapo kutatokea ugomvi ndani ya ndoa na kushauri kuwaona viongozi wa dini, Serikali, Wazee au wazazi kwa kutafuta suluhu

Chanzo East Africa Tv

The post Mume amchinja mkewe kisa tendo la Ndoa, Katavi appeared first on Bongo5.com.