Mbunge wa Iringa Mjini aliyemaliza muda wake kupitia CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa aliamua kuwasikiliza wazee wa Mkoa huo, hii ni baada ya wao kumfuata na kumuomba aachane na nia yake ya kugombea Urais abaki kutumikia jimbo hilo.

Msigwa ametoa kauli hiyo hivi karibuni  mara baada ya yeye kutochukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kumteua ili aweze kugombea Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao.

"Nililazimika kutoendelea na mchakato wa Urais sababu Wazee na watu wa Iringa waliniomba sana na kunisihi bado niendelee kukaa kwenye jimbo , kwahiyo niliona nisikilize wazee na usia wao, nikaona niwapishe hawa wengine waendelee Mungu akiruhusu wakati mwingine nitarudi" amesema Msigwa.