Mfanyabiashara, Mohammed Dewji, maarufu kwa jina la MO amemuomba Rais John Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa.

“Leo nimeamua kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa kuwa: Uwanja wa Benjamini William Mkapa,” aliandika MO katika ukurasa wake wa Twitter.