WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe .Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe ametuma ujumbe tata kwenye ukurasa wa twitter ikiwa ni siku kadhaa kutangaza nia yake ya kutaka kuwania nafasi ya urais kupitia chama cha upinzani anachotarajia kukutangaza hivi karibuni.

Ambaye alirejesha kadi ya uwanachama wa chama chake wa awali CCM ameandika ujumbe huo leo julai 9, 2020 akidai kuwa yeye sio wa kudhalauliwa hukuakiwa hajaweka wazi ujumbe huo ametuma kwa nani hasa.

“Usinidharau kwa ajili mwembamba.. Mimi ni kitawi cha mkomamanga… Sitapiki nyongo nikailamba……! “ ameandika Membe.

Ikumbukwe siku kadha zilizopita akizungumza na idhaa ya kiswahili ya shirika la utangazaji la BBC, Membe amenukuliwa akisema chama chake cha zamani (CCM) kimekuwa kikiwadharau baadhi ya viongozi wa zamani wa chama hicho na serikali.