Manchester City wametakiwa kuweka mezani kitita cha pauni milioni 65 kwa ajili ya beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, 29, ambaye anauhishwa na taarifa za kuhamia Liverpool na Manchester United na awali alikuwa na thamani ya pauni milioni 80. (Daily Mirror)
Manchester City inamtazama mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez, 22, kama mchezaji muhimu katika kuchukua nafasi ya Sergio Aguero,32. (Sky Sports)
Hata hivyo, Martinez yuko ukingoni kumalizana na hatua za uhamisho kuelekea Barcelona. (Marca)
Bayern Munich inatafuta pauni milioni 40 kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa zamani Thiago Alcantare, Mhispania ,29. (Sport Bild via Daily Mirror)
Bayern wanafikiriwa kujitoa katika kinyang’anyiro cha kumnasa kiungo Kai Havertz,21 anayekipiga na Bayer Leverkusen. (Sport Bild, via Daily Mail)
Everton, Atletico Madrid na Bayern Munich wanatarajiwa kuweka nia ya kumnyakua winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha msimu huu, huku Newcastle pia ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo,27. (Daily Mail)
Southampton wana matumaini ya kupata mkataba wa kudumu wa pauni milioni 10 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Totteham, Muingereza Kyle Walker-Peters,23, ambaye anakipiga Saints kwa mkopo tangu mwezi Januari (Sun)
Kocha wa Southamton Ralph Husenhuttl amekataa kufanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa kubadilishana kiungo wa kati Pierre-Emile Hojbjerg,24, na Walker-Peters. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Birmingham Jude Bellingham,17 amekubali kuhamia Borussia Dortumund kwa kitita cha pauni milioni 22.5. (Bild)
Kiungo wa Ghana Thomas Partey,27, anaripotiwa kujiandaa kusaini mkataba mpya na Atletico Madrid, ambayo imemuahidi kumpa mshahara mara mbili zaidi. (Ghana SoccerNet,via Daily Mail)
Pep Guardiola amefungua mlango kwa ajili ya kiungo wa kati wa Aston Villa Douglas Luiz,22, kurejea Manchester City baada ya kufuguliwa kwa dirisha la usajili mwezi Julai. (Birmingham Mail)
Kiungo wa kati wa Liverpool Adam Lallana,32, ambaye anawaacha miamba hiyo kwa uhamisho huru msimu huu, ananyemelewa na Leicester,Burnley na Brighton. (Daily Star)
Beki wa Tottenham Danny Rose,30, ameendelea kuwa na matumaini ya kuufanya mkataba wake kuwa wa kudumu katika klabu ya Newcastle, huku kukiwa na taarifa za kuhusishwa kwake na Lazio (Newcastle Chronicle)
Middlesbrough wanaelekea kukubali kumpoteza beki wao wa kulia, Muingereza Djed Spence,19 msimu huu wakati vilabu kadhaa vya primia wakiwemo Tottenham, West Ham na Brighton wakijiandaa kuongeza kasi ya kumnasa mchezaji huyo. (ESPN)
Kiungo wa Everton Mo Besic,27, atakuwa tayari kuuzwa au kuondoka kwa mkopo msimu huu. (Liverpool Echo)
Portsmouth inatazamia uhamisho kwa mkopo wa beki wa kushoto wa Brighton Alex Cochrane,20. (Argus)
Kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo hana uhakika iwapo mshambuliaji Raul Jimenez,29, atakosa mechi yoyote kwasababu ya kutarajia kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza. (Express and Star)
The post Mbadala wa Aguero ndani ya Man City apatikana appeared first on Bongo5.com.