SELEMANI Matola, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba ambao ni mabingwa mara tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2019/20 katika Ligi Kuu Bara amesema kuwa ishu yake ya kuibukia Azam FC haijafi ka mezani.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya Matola ambaye ana uzoefu na ligi ya Bongo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Matola alisema: “Mimi ni kocha wa Simba kwa sasa na ndipo ambapo ninafanya kazi kuhusu kutakiwa na Azam FC bado sijapata taarifa na ikiwa watakuja ndipo nitazungumza ila kwa sasa nipo Simba.”

Azam FC kwa sasa inapambania kurejesha makali yake kwa kuwa msimu huu imeweka rekodi ya kuboronga kwenye mashindano yote iliyoshiriki.

Iliyeyeyusha taji la Kagame, taji la Mapinduzi, taji la Kombe la Shirikisho na sasa inapambania kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili.

Ofi sa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ameliambia gazeti hili kuwa mpango mkubwa uliopo ni kuboresha kikosi kizima kwa ajili ya msimu ujao ikiwa ni pamoja na benchi la ufundi.

Lunyamadzo Mlyuka | Dar es Salaam