Anaandika @stevenyerere2

Kupitia ukurasa wake wa Instagram

"Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri

Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao walinipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri

Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,

Ukimbini tulipoingia,
Sera kuwamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,

Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Walichonifanya wajumbe sikuamini,
Wajumbe sio watu wazuri

Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Ningejinyonga ningekuwa kihoja,

Wajumbe sio watu Waziri" STEVENE NYERERE