Marekani imeitaka China kufunga ubalozi wake mdogo katika jiji la Texas katika Jimbo la Houston, Wizara ya Mambo ya nje ya China imesema ikilaani vikali uamuzi huo na kutishia kuchukua hatua za kulipiza kisasi.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila siku, msemaji wa wizara ya mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin, amesema Beijing iliarifiwa ghafla kuhusu hatua hiyo Jumanne wiki hii. Hata hivyo hakutoa sababu za Marekani kuitaka China kufunga ubalozi wake mdogo huko Texas.

Mamlaka nchini Marekani imeipa China siku tatu kuwa imefunga ubalozi wake mgodo Texas, Wang Wenbin amesema.

"Hatua ya Marekani kufunga ubalozi wa China huko Houston, bila hata hivyo kuishirikisha serikali ya Beijing, katika kipindi kifupi kama hiki ni muendelezo wa hatua za hivi karibuni za Marekani dhidi ya China," Wenbin ameongeza.

"Tunaiomba Marekani kufuta uamuzi huo mbaya mara moja. Kama itaendelea kushikilia uamzi wake huo mbaya, China italipiza kisasi kwa kuchukuwa hatua kali, " amebaini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani Morgan Ortagus, amesema  amri hiyo ililenga kulinda hakimiliki za Marekani na taarifa za faragha za raia wa Marekan