Kundi la Waandamanaji limeangusha sanamu ya Christopher Columbus na kuitupa kwenye maji katika bandari mjini Baltimore hapo jana usiku

Wimbi la maandamano lilianza nchini humo, baada ya Polisi kumuua Mmarekani mweusi, George Floyd Mei 25. Maandamano hayo yalienea katika nchi kadhaa duniani

Waandamanaji wamekuwa wakitaka kuondolewa kwa masanamu mengi ya kihistoria yenye utata, ya watu wanaoelezwa kuhusika na ukandamizaji kwa karne kadhaa

Columbus anayesifiwa kwa kuligundua bara la Amerika, hivi karibuni wanahistoria na wanaharakati wamesema alihusika pia katika utumwa, unyonyaji na ukandamizaji pamoja na umwagaji damu wa watu