Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wamelazimika tena kukaa majumbani na kuepukana na usafiri kufuatia masharti ya kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona.

TFSCB's rapid support to help countries respond to the COVID-19 ...

India ni miongoni mwa nchi ambazo zimerudisha masharti ya kuzuia usafiri wa watu mnamo wakati maambukizi ya virusi vya corona yanazidi kuongezeka.

Tangu mwanzo wa mwezi Julai, takriban maambukizi mapya milioni 2.5 yamerekodiwa ulimwenguni kote, idadi hiyo ikiwa maradufu ya maambukizi yaliyotokea katika muda wa wiki sita kabla.

Hayo ni kulingana na ujumuishaji wa takwimu rasmi uliofanywa na shirika la habari la AFP. Nchini Marekani, jumla ya maambukizi 63,262 yamerekodiwa katika saa 24 zilizopita.

Kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha John Hopkins jumla ya watu 850 pia wamefariki nchini humo katika saa 24 zilizopita kutokana na COVID-19.

Takriban watu milioni 13 ulimwenguni kote wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo na zaidi ya watu 570,000 wamefariki.

The post Mamilioni ya watu walazimika kukaa tena majumbani kufuatia Corona appeared first on Bongo5.com.