Ufisadi huo unahusiana na kashfa ya mabilioni ya dola yaliyokuwa yametolewa na serikali kwa ajili ya mradi wa maendeleo.
Fedha za mradi huo ziliibiwa na kuelekezwa katika matumizi binafsi, yakiwemo ununuzi wa magari ya anasa na kazi za sanaa zenye gharama kubwa.
Hukumu hii dhidi ya Najib Razak ilichukuliwa kama kipimo kwa utawala wa sheria nchini Malaysia, kwani imetolewa miezi mitano tu baada ya muungano unaokijumuisha chama cha Razak kushinda uchaguzi, ambapo wengi walihofu kuwa ushindi huo ungeshawishi uamuzi wa mahakama.
Akitoa hukumu hiyo leo, jaji wa mahakama ya juu ya Malaysia amesema upande wa waendeshamashtaka umeweza kutetea hoja yake vyema na kuondoa mashaka yote juu ya hatia ya Razak.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la mahakama mjini Kuala Lumpur mchana wa Jumanne (29 Julai), Najib alisema kuwa mashitaka dhidi yake yalikuwa ya kisiasa na kwamba hahusiki na kadhiya hiyo ya ubadhirifu wa kiasi cha mabilioni ya dola yaliyotoweka kwenye mfuko wa maendeleo wa serikali, maarufu kama kashfa ya 1MDB:

