Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akifungua Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichokutana leo Julai 04,2020 Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. wa pili kulia ni  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe wa kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakipitia Mafaili kabla ya kuanza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichokutana leo Julai 04,2020 Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar .  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Baadhi ya Wajumbe wa kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar  leo Julai 04,2020.