Julai 29,2020, Mahakama mkoani Manyara imeyataifisha Madini ya Tanzanite gramu 132.64 yenye  thamani ya shilingi Milioni 18,446,894.14 yaliyokutwa kwa mfanyabiashara wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, kinyume na Sheria. 


Mfanyabiashara huyo  wa madini ya Tanzanite wilayani humo Lucas Liaseki amekamatwa na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara mbele ya hakimu mkazi Simon Kobelo baada ya kujaribu kutorosha madini ya Tanzanite katika geti la ukaguzi wa madini hayo Mirerani. 


Wakili wa serikali mwandamizi ambaye pia ni mkuu wa mashtaka mkoa wa Manyara Mutalemwa Kishenyi amesema mfanya bishara huyo alikamatwa kwa kosa la kutokuwa na kibali cha ambapo serikali imeyataifisha. 


Aidha amesema mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi 12 na kumuamuru asifanye kosa lolote kwa kipindi hicho.