Baada ya ushindi wa hapo jana wa Real dhidi ya Villarreal na kipigo cha Barcelona cha magoli 2 – 1 mbele ya Osasuna kimewafanya madrid kutawazwa kuwa mabingwa ramsi wa La Liga.

Real Madrid is 19-20 Spanish champion | En24 News

Real Madrid imejitangazia ubingwa wa La Liga huku ikiwa imesalia na mechi moja mkononi baada ya kuwashushia kipigo cha magoli 2 – 1 Villareal katika uwanja wa Alfredo Di Stefano uliokuwa hauna mashabiki.

Mabao ya ushindi yakifungwa na Karim Benzema dakika ya 29 na lile la penati dakika ya 77 ya mchezo ambalo liliwatangazia ubingwa.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane a.k.a Zizou  anasema kwamba ushindi wa taji la kwanza na Real Madrid baada ya kipindi cha miaka mitatu umemfurahisha zaidi ya kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya.

”Hii ni bora zaidi ya chochote kile. Inahitaji jitihada ya hali ya juu ili kucukua kombe la La Liga”, alisema mkufunzi huyo wa Real Madrid.

”Hii leo ni mojawapo ya siku bora zaidi kwangu mimi kama mwalimu. Baada ya kila kilichotokea, likizo ya miezi mitatu, ni vyema tulichofanikiwa.”

Kwa Real Madrid mataji ya La Liga yamekuwa machache ukilinganisha na yale ya klabu bingwa Ulaya muongo huu na hili likiwa taji lao la tatu katika kipindi cha misimu yao tisa.

Walishinda mataji matatu mfululizo katika makombe ya Ulaya katika kipindi cha kwanza cha Zidane lakini walikuwa wakimaliza katika nafasi ya tatu tangu waliposhinda taji hilo kwa mara ya mwisho, ambapo Bareclona wamekuwa wakitawazwa kuwa mabingwa.

The post Madrid mabingwa wapya Hispania 2019/20, Zizou adai taji la La Liga ni tamu zaidi ya lile la UEFA  appeared first on Bongo5.com.