Kumekuwa na ripoti kwamba hospitali za umma nchini Madagascar zimejaa na zimekuwa zikiwalaza wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi. Taifa hilo kwa sasa lina takriban wagonjwa 7000 wa Covid-19. Rais Andry Rajaolina mapema mwezi huu aliweka masharti ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo kufuatia kuongezeka kwa maradhi hayo.
Mnamo mwezi Aprili, alizindua dawa ya mitishamba ya maradhi ya Covid-19 ambayo ilisambazwa nchini humo. Mizigo kadhaa ya dawa hiyo ya Covid Organic pia ilitumwa kwa makumi ya mataifa barani Afrika.
Hatahivyo uwezo wa kinywaji hicho umepuuziliwa mbali na wataalam wa Afya nchin NIgeria na DR Congo mataifa ambayo yalifanyia majaribio dawa hiyo.