Shirika la Afya Duniani WHO limeripoti kwa siku ya pili mfululizo juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona duniani, huku jumla ya visa vya vipya ikipindukia 259,000 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya kila siku ya WHO maambukizi makubwa siku ya Jumamosi yamerikodiwa nchini Marekani, Brazil, India na Afrika ya Kusini.

Takwimu za siku ya Ijumaa zilionesha kulikuwa na visa vipya 237,000 huku idadi ya watu wanaokufa kwa siku kutokana na ugonjwa wa COVID-19 imepanda katika siku za karibuni ikilinganishwa na miezi wiki chache zilizopita.

Kulingana na tarakimu zilizojumuishwa na shirika la habari la Reuters, visa vya virusi vya corona duniani vilipindukia milioni 14 siku ya Ijumaa na janga hilo tayari limewauwa karibu watu 600,000 katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

The post Maambukizi ya COVID-19 kwa siku yapanda ulimwenguni – WHO appeared first on Bongo5.com.