Meneja Masoko wa startimes ,David Malisa  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya kutoa  zawadi mbalimbali kama Smart Tv, vingamuzi na vifurushi mbali mbali kwa wateja watakao bashiri na M-bet promosheni hio itajulikana kama Cheza na M-bet , shinda na Star times.kushoto kwake ni Meneja masoko kutoka M-bet  Allen Mushi, mapema leo Jijini Dar es salaam.
Meneja masoko kutoka M-bet  Allen Mushi,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari   (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa promosheni ya cheza na M bet ambapo wateja watajishindia zawadi mbali mbali kutoka startimes ,Mapema Leo Jijini Dar es salaam .Meneja Masoko wa startimes ,David Malisa akimkabidhi zawadi ya kingamuzi mmoja wa washindi wa Promosheni ya Cheza na MBET mara baada ya uzinduzi mapema leo patika ofisi za Startimes Jijini Dar es salaam .
Washindi  mbali mbali wa zawadi kutoka startimes wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kukabidhiwa Zawadi zao katika promosheni ya Cheza na MBET Mapema leo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam .
***************

M-Bet kwa kushirikiana na Kampuni ya kutoa huduma ya matangazo ya runinga ya StarTimes nchini Tanzania, leo imezindua promosheni ya kutoa  zawadi mbalimbali kama Smart Tv, vingamuzi na vifurushi mbali mbali kwa wateja watakao bashiri na M-bet promosheni hio itajulikana kama Cheza na M-bet , shinda na Star times.
 
Akiongea na waandishi habari jijini Dar es Salaam baada ya hafla ya uzinduzi huo   Meneja masoko kutoka M-bet  Allen Mushi, amesema kuwa shindano hilo linalelnga kuwa zawadia wateja wote wa M-bet  Tanzania watakao jisajili na kubashiri kwa M-bet . M-Bet inaendelea kutoa washindi mbali mbali katika michezo ya kubashiri kwa mtandao.

Kwa upande wa Star Times, Meneja Masoko,David Malisa alisemaKampuni hiyo ya StarTimes ni moja wapo ya makampuni makubwa zaidi ya kutoa huduma ya matangazo, ya runinga nchini Tanzania, hususan katika ngwe ya michezo kwa kuonesha ligi mbali mbali kama La Liga , Bundesliga  nk. Ushirikiano na M-bet ni endelevu katika kutoa burudani kwa watanzania wote.
 
Shindano hilo litakuwa likitoa zawadi hizi kila wiki,mteja anachohitajika kufanya ni kusijali na kucheza na M-bet kwa tovuti ya M-bet.co.tz.