Katika kura za maoni za Jimbo la Kyela, Ally Mlagila Jumbe (Kinanasi), Mwenyekiti wa CCM Wilaya ameibuka kidedea kwa kupata kura 502, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Hunter Mwakifuna aliyepata kura 288.
Aidha, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo amekuwa wa tatu kwa kupata kura 252.
Uamuzi unabaki kwa Kamati Kuu kumteua wa kuwakilisha Jimbo katika Uchaguzi Mkuu 2020.
The post Kyela: Ally Mlagila Jumbe aongoza, Dkt. Mwakyembe ashika nafasi ya tatu appeared first on Bongo5.com.