Picha za jua zilizopigwa kutoka umbali wa kilomita milioni 77 tu ni za hivi karibu kuwahi kupigwa kwa karibu zaidi kwa kutumia kamera. Picha hizo ni kutoka Shirika la Anga la Ulaya kupitia setilaiti ya kutazama jua iliyorushwa mapema mwaka huu.
Miongoni mwa vilivyonaswa ni pamoja na muonekano wa mwako kidogo.
Ni mamilioni ya mwako wa jua ambao kawaida huonekana kwa kutumia darubini kutoka ardhini.
Ingawa kile ambacho bado hakijabainika ni ikiwa mwako huu unapatikana kwa njia ile ile ya kawaida.
Lakini mwako huu mdogo mno huenda unahusika na mchakato wa joto unaofanya eneo la nje la jua au tabaka la mzingo kuwa na joto zaidi.
“Jua lina eneo lililobaridi la takriban selsiasi 5,500 na limezingirwa na eneo lenye joto kali zaidi ya selsiasi milioni,” ameelezea mwanasayansi Daniel Müller.

Setilaiti ya Shirika la Anga la Ulaya ilirushwa kupitia roketi kutoka eneo la Cape Canaveral Marekani Februari.
Lengo lake lilikuwa ni kubaini siri iliyopo katika mzunguko wa jua.
Jua lina makujumu mengine mbali kabisa na kutoa mwanga na joto.
Mara nyingi huwa kuna chembechembe zinazoruka kutoka uga sumaku wa jua kupitia kwenye setilaiti na kuharibu mawasiliano ya redio.
Na uvumbuzi huu unaweza kusaidia wanasayansi kutabiri vizuri muingiliano huu.
“Hali ya hivi sasa ya ugonjwa wa virusi vya corona imeonesha umuhimu wa kuwa na mawasiliano na setilaiti ni sehemu ya mawasiliano,” amesema Caroline Harper, mkuu wa Shirika la Anga la Uingereza.
“Kwa hiyo ni muhimu sana kuendelea kufahamu mengi kuhusu jua ili tuweze kubashiri hali ya anga iliyopo kwenye jua kama tulivyojifunza kubashiri hali ya hewa hapa duniani.”

Chombo cha kuchunguza jua kimewekewa mfululizo wa mizunguko karibu na jua – na hatimae itasababisha kuachana kwa umbali usiozidi kilomita milioni 43.
Picha zilizooneshwa Alhamisi zinatoka eneo la karibu la jua linalofahamika kama perihelion kwa Kiingereza. Hili lilitokea katikati ya Juni ndani ya mzunguko wa nyota ya Venus yaani Zuhura.
Kwa ulinganisho, Dunia ipo takribani kilomita milioni 149 sawa na (maili milioni 93) kwa wastani kutoka kwenye jua.
Wakati ambapo picha za karibu zaidi za jua kuwahi kupigwa zimepatikana sio eti ndio mafanikio makubwa kufikiwa.
Itachukua miaka kadhaa kabla ya chombo cha jua kupiga picha zingine za karibu zaidi umbali wa kilomita milioni 48 kutoka uso wa jua.
Wakati mchakato huo unaendelea, kupitia Shirika la Anga la Ulaya pamoja na nguvu za uvutano za nyota ya Zuhura, chombo kinachochunguza jua kitakuwa kinajiondoa kwenye nyota ili kiweze kuona kwa urahisi zaidi, takaba la jua lenye mashimo ambalo ni baridi linalo badilika badilika.
Na katika eneo hilo, huenda hatimae dunia ikafahamu mambo ya msingi kuhusu nguvu za sumaku za jua.
“Tunajua kwamba uga sumaku wa jua ndio unaosababisha yote yanayotokea kwenye jua, lakini hatujui uga sumaku huu jinsi unavyotengenezwa,” amesema mwanasayansi kutoka Taasisi ya Utafiti wa mfumo wa jua.
“Tunafikiria kwamba huenda ikawa ni mfano wa mota inayofanya hivyo ndani ya jua, kama ilivyo ndani ya dunia. Lakini hatujui jinsi inavyofanyakazi.”
Holly Gilbert, mwanasayansi wa Shirika la Anga la Marekani anayeshirikiana na Shirika la Anga la Ulaya kwenye mradi huu wa kuchunguza jua, ana matumaini makubwa na hatua zitakazopigwa siku za usoni kisayansi.
“Ikiwa tayari tumeshabaini kitu kwa na picha za kwanza tu za mwanga tulizopiga, fikiria ni kitu gani tutakachogundua tutakapokaribia zaidi jua, na tutakapotoka nje ya ekliptiki. Ni jambo linalosisimua sana.”
Chanzo BBC.
The post Kwa mara ya kwanza hizi ndio picha za Jua zilizopigwa kwa karibu zaidi appeared first on Bongo5.com.