"Mungu wetu ni mwema sana, katika mazingira ya kawaida sikutakiwa niwe hai, nimerudi nyumbani kwetu, ni miaka mitatu kasoro mwezi ifike ile siku ambayo hata sikumbuki hata niliondokaje, miaka mitatu ambayo ilikuwa ni migumu sana" - Tundu Lissu

"Mkiniona nimevaa hivi unaweza usielewe sana kungekuwa na uwezekano wa kuvua magwanda haya, wote mtakimbia kwa sababu huu mwili ukiachia kichwa na uso, huu mwili ni ramani za makovu ya risasi na visu vya Madaktari, huu mwili una vyuma vingi" - Tundu Lissu

"Huu Mguu wa kulia umejaa vyuma kuanzia kwenye Goti hadi kwenye Nyonga, vingine vipo kwenye mkono wa kushoto na Mkono wa kushoto haunyoki, kuna Risasi iko chini ya Mgongo Madaktari walisema ibaki hapo hapo ni salama zaidi kuliko kuitoa" - Tundu Lissu