Kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kichonge Mahende Masero, ambaye ametia nia ya kugombea jimbo la Tarime Mjini alizua gumzo akiwa anachukua fomu na kuirejesha akiwa kwenye usafiri wa mkokoteni.

Masero ambaye ni kada wa CCM Ijumaa Julai 17, 2020 wakati akirejesha fomu alitumia usafiri wa mkokoteni huku bodaboda zikimsindikiza.

Baadhi ya watu walimshangaa alivyokuwa akiendeshwa na mkokoteni huo.