Baada ya kifo cha Mwanasiasa mkongwe, Balozi Job Lusinde (90) ambaye alikuwa mmoja wa baraza la kwanza la mawaziri la Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru, kufariki dunia alfajiri ya siku ya Jumanne, Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Familia ya Lusinde na Malecela imesema taratibu za mazishi zinaendelea katika makazi yake, Kilimani, jijini Dodoma. Lusinde ni kaka wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, John Malecela.

Lusinde aliyezaliwa Oktoba 9, 1930, aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka 1965 na ni miongoni mwa watu waliofanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Julius Nyerere kama Waziri wa Serikali za Mitaa mwaka 1961. Pia, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1984.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salam za Rambirambi kwa familia an Watanzania wote kwa kusema kuwa:-

“Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde. Nawapa pole Familia, wana Dodoma na Watanzania. Nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee wa Dodoma. Pumzika salama Mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri.”

The post JPM kuhusu kifo cha balozi Lusinde, Pumzika kwa amani mtani wangu appeared first on Bongo5.com.