Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha sherehe za Mashujaa zilizopaswa kufanyika tarehe 25.07.2020 jijini Dodoma.

Pamoja na kauhairsha sherehe hizo, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kutumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea Mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya Nchi yetu na hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali zikiwemo mtu mmojammoja na familia.

Mhe. Rais Magufuli amewatakia heri Watanzania wote kuelekea siku hiyo na amewataka kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.

The post JPM aahirisha sherehe za mashujaa, Watanzania tumieni siku hiyo kuwaombea mashujaa wote appeared first on Bongo5.com.