Mahakama ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemuhukumu Clement Salama(19) kutumikia kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kumbaka na kumpatia ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 17.

Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi wilayani humo, Mlisho Kimbeho, amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Mwezi April mwaka huu kisha kufikishwa Mahakamani kwa makosa mawili ambayo ni ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi.

Baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha, mshtakiwa alikiri wazi kutenda kosa hilo huku akiiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwani bado ni kijana mdogo nani tegemezi kwao.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ramadhani Rugemalira, amesema kosa hilo ni kinyume na sharia kifungu 130(1) 2e na kifungu 131 (1) cha sharia ya adhabu kwa kumbaka mwanafunzi kisha kumpatia ujauzoto na kumsababishia kutoendelea na masomo yake , na kusema Mahakama inamuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 jela.