Kesi mpya inayomkabili aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir ilianza jana Jumanne, Julai 21. Omar al-Bashir aliondoka madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Aprili 2019.

Omar al-Bashir alihukumiwa mnamo mwezi Desemba mwaka jana kifungo cha hadi miaka miwili kwa kosa kosa la rushwa.

Mapinduzi ya Omar El Bashir yalifanyika mwaka 1989 dhidi ya Sadiq al-Mahdi, Waziri Mkuu wa wakati huo wa Sudan na kushika hatamu za uongozi wa nchi.

Baada ya al-Bashir kuiongoza Sudan kwa mkono wa chuma kwa miaka 31, sasa anatarajia kujibu tuhuma zinazomkabili mbele ya mahakama maalumu inayoundwa na mkuu wa Mahakama Kuu na majaji wawili kutoka Mahakama Rufaa.

Anatuhumiwa kukiuka agizo la katiba na anakabiliwa na adhabu ya kifo. Omar al-Bashir atahukumiwa na watu wengine 16, raia wa kawaida na askari, akiwemo Makamu wa Rais Taha na Jenerali Bakri Hassan Saleh.

Hata hivyo Mohamed Al Hassan Al Amin, mmoja wa wanasheria wa Omar al-Bashir, anaema kesi dhidi ya mteja wao ni ya kisiasa.