Vizazi vitatu vya familia maarufu inayoshiriki katika filamu za Bollywood vimekutwa na virusi vya corona kulingana na maafisa katika jimbo la Maharashatra nchini India.

Matokeo siku ya Jumapili yalionesha kwamba muigizaji wa kike Aishwarya Rai Bachchan , ambaye aliwahi kushinda tuzo la malkia wa urembo duniani na mwanawe Aaradhya, mwenye umri wa miaka minane waliambukizwa virusi hivyo.

Mumewe Abhishek na baba mkwe Amitabh , wote waigizaji walipelekwa hospitalini siku ya Jumamosi wakiwa na virusi hivyo. Wote wawili walidaiwa kuwa na dalili chache za corona.

Abhishek Bachchan alichapsha ujumbe wa Twitter kwamba watasalia hospitalini hadi pale madaktari watakapoamua.

Aishwarya Bachchan mwenye urmi wa miaka 46 ni mojawapo wa waigizaji maarufu wa Bollywood nchini India na ughaibuni, wakishiriki katika filamu kadhaa za Bollywood na Hollywood.

Alishinda taji la malkia wa urembo duniani 1994 na ni balozi wa shirika la Umoja wa Mataifa UNAIDS .

Mwaka 2003 alikua raia wa kwanza wa India kuwa mwanachama wa jopo la Tamasha la filamu za Cannes . Aishwarya na mwanawe wanadaiwa kuwa hawana dalili.

Mumewe alituma ujumbe wa Twitter akisema kwamba wanajitenga nyumbani

Wengi wajitokeza kuwatumia risala za kupona kwa haraka

Siku ya Jumamosi Amitabh Bachchan aliambia mamilioni wa wafuasi wake wa twitter kwamba amekutwa na corona.

”Nimekutwa na corona , nikapelekewa hospitalini, hospitali inawajuza watawala , familia na wafanyakazi wanafanyiwa vipimo, matokeo yakisubiriwa”, aliandika.

Bachchan mwenye umri wa miaka 77 amehusishwa na filamu 200 katika kipindi cha miongo mitano.

Amitabh Bachchan
Bachchan ameshinda tuzo chungu nzima tangu alipojipatia umaarufu miaka ya 70

Yeye na Abhishek, mwenye umri wa miaka 44 walichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya Nanavati mjini Mumbai siku ya Jumamosi. Abhishek aliwaelezea wote kuwa na dalili chache.

Amitabh kwa sasa ametengwa katika kitengo kimoja cha hospitali hiyo ,kitengo cha habari cha ANI kiliripoti kikimnukuu afisa mmoja wa mahusiano ya umma katika hospitali hiyo.

Aliwataka wale wote waliokaribiana naye katika kipindi cha siku 10 zilizopita kupimwa. Maafisa wa baraza la mji wa Mumbai tayari wameweka mabango nje ya nyumba ya muigizaji huyo , wakitaja eneo hilo kama lililotengwa.

Habari hizo zimesababisha kutumwa kwa ujumbe wa heri njema katika mitandao ya kijamii. Miongoni mwa wale waliotuma ujumbe huo ni mwigizaji wa kike Sonam K Ahuja na mchezaji wa zamani wa mchezo wa magongo Irfan Pathan.

Wafuasi wa familia hiyo wamekuwa wakutuma rambi rambi kwa familia hiyo kuwatalka wapone kwa haraka
Wafuasi wa familia hiyo wamekuwa wakutuma rambi rambi kwa familia hiyo kuwatalka wapone kwa haraka

”Kwa mpendwa Amitabh najiunga na taifa zima kukutakia upone kwa haraka! Wewe ni mtu unayependwa na mamilioni ya watu nchini humu. Tutakulinda. Tunakutakia upone kwa haraka”, alisema waziri wa Afya nchini India Harsh Vardhan.

Bachchan amekuwa muigizaji mkuu katika filamu kuu kama vile Zanjeer na Sholay.

Tangu kupanda kwa umaarufu wake 1970, ameshinda mataji kadhaa ikiwemo mataji manne ya National Film Awards na mengine 15 ya Filmfare Awards. Ufaransa pia imemtuza taji lake kubwa la Legion of Honour, kwa mchango wake katika filamu.

Mbali na filamu Bachhan aliingia katika siasa na alichaguliwa kama mbunge 1984 kwa agizo la waziri mkuu Rajiv Gandhi. Lakini alijiuzulu miaka mitatu baadaye akichukizwa na kadhfa za ufisadi katika serikali ya Ghandhi.

Katika miezi ya hivi karibuni , amekuwa maarufu katika kuisaidoa serikali kupitisha ujumbe wake katika vita dhidi ya corona. Idadi ya mambukizi nchini India iliongezeka siku ya Jumapili , huku jumla ikipanda hadi 850,000, ikiwa ndio idadi kubwa duniani. Kumekuwa na malalamishi kuhusu ukosefu wa vifaa vya kupima na maafisa wa afya.

The post INDIA: Muigizaji Amitabh Bachchan na familia yake wakutwa na virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.