Na Mwandishi Wetu, Korogwe Tanga

Idadi Kubwa ya ya shule Wilayani Korogwe mkoani Tanga zipo katika wasi wasi wakutofikia malengo waliyojiwekea na wazazi kutokana na likizo ndefu ya kukakaa nyumbani iliyotokana na Mlipuko wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Covid 19.

Hayo yameelezwa na Wazazi pamoja na Walimu wa shule mbalimbali hapa Korogwe kutokana na jinsi walivyoweza kuwa pokea watoto na maisha waliyokuwa wanaishi nyumbani wskati wa mapumziko hayo.


Nasibu Ponda ni Mmoja ya wazazi wanaoishi wilayani hapa katika kata ya Chekelei anasema kuwa wazazi na walimu walijiwekea malengo ya kupandisha ufaulu katika shule zao hali imekuwa tofauti mara baada ya mlipuko wa ugonjwa huu.

"Malengo tuliyojiwekea Wazazi na Walimu ayatofikiwa kutokana na Changamoto za usimamizi wa ufundishaji kwa wanafunzi kipindi cha likizo hali iliyofanya wanafunzi wengi kushuka viwango" anasema Ponda.

Anasema kuwa wazazi wengi waliwageuza watoto kama wasaidizi wa kazi na kushindwa kuwapa muda wa kujisomea au kufanya mazoezi waliyopewa shuleni.

Degratius Mapima ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Mlangai anaweka wazi kuwa inahitajika nguvu ya ziada hili shule ziweze kufikia malengo waliyojiwekea awali na wazazi katika kupandisha ufaulu katika shule zao.

Anasema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wamerudi kama wanaanza upya na kutaja kuwa hasa wale wa kidato cha kwanza wengi wao wamekuja na madaftari mapya na ukiwauliza ya zamani yako wapi awaelewi.

Nae Mwalimu wa Taaluma wa shule ya Sekondari Mlangai, Remigius Rutahiwa anasema kuwa wao kama walimu wamekutana na changamoto kubwa ya watoto kushuka kitaaluma mara baada ya kurejea shuleni.

"Wakati wa likizo tuligawa Majaribio kupitia ofisi za watendaji ambazo tulitaka kila mtoto aweze kufanya na kurejesha lakini cha ajabu ni asilimia 30% tu ya wanafunzi wote waliopatiwa majaribio ndio wameweza kufanya na kurejesha shuleni" anasema Mwalimu Rutahiwa

Anasema mbali na kushuka kitaaluma baadhi ya wanafunzi wamerudi na mabadiliko ya kitabia na kuja na tabia za mtaaani hasa watoto wa kiume.

Anaweka wazi kuwa asilimia zaidi ya 80%  ya Vijana wa kiume walirudi na minyoo ya mitindo huku wengine wakija wameweka wei na wengine kunyia kiduku hali iliyiwalizimu kuwaamuru wote wanyoe upara.

Anasema wao kama walimu wamejipanga kwa kuhakikisha wanafata
Muongozo wa kuhakikisha wanafundisha kwa kuongeza muda wa ziada licha ya kukabiliwa na changamoto za uchache wa walimu .
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari mlangai wakifatilia vipindi Darasani.