Kwa mara ya kwanza tuzo za Ballon d’or hazitofanyika tangu ilipoanzishwa mwaka 1956 kutokana na janga la corona kuathiri shughuli za michezo mwaka huu.

Lionel Messi

Kwa mara ya kwanza tuzo za Ballon d’or hazitofanyika mwaka huu tangu zilipoanzishwa mwaka 1956 kutokana na janga la corona kuathiri shughuli za michezo mwaka huu.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi alishinda tuzo hiyo mara ya sita mwaka uliopita, akimshinda Cristiano Ronaldo aliyeshinda mara tano.

Katika kipindi cha muongo mmoja nyota hao wawili wamekuwa wakibadilishana tuzo hiyo, ingawa mwaka 2018 ilichukuliwa na Luka Modric.

Ballon d’Or, inayotolewa na jalida la soka la Ufaransa, imekuwa kila mwaka ikitoa tuzo hiyo tangu Sir StanleyMatthews alipokuwa mshindi wa kwanza miaka 64 iliyopita.

Baada ya taarifa hii ya kutokuwepo kwa tuzo hizo kubwa duniani klabu ya Barcelona kupitia ukurasa wake wa Twitter wamepost picha ikumuonyesha Lionel Messi akiwa na tuzo zake 6 na kuandika kwamba:-

“We understand. Besides, everyone knows who the best is.”

Wakimaanisha kuwa “Wote Tunaelewa, Mbali na hilo, kila mtu anajua nani bora.”

The post Hii ndio sababu za tuzo ya Ballon d’or kufutwa mwaka huu, Barcelona watoa kauli hii appeared first on Bongo5.com.