Waziri wa fedha wa Saudi Arabia amesema leo kuwa hakuna uamuzi wa mwisho uliofikiwa juu ya iwapo mkutano wa kilele wa kundi la mataifa ya G20 utafanyika kwa kukusanyika mahali pamoja ama utafanyika kwa njia ya vidio na suala hilo bado linajadiliwa.

Mkutano wa kilele wa viongozi wa G20 umepangwa kufanyika mwezi Novemba na Saudi Arabia ni mwenyeji wa mkutano huo wa kila mwaka wa wawakilishi wa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani.

Waziri wa fedha Mohammed al-Jaddaan alikuwa akizungumza katika tukio la kampuni ya masuala ya fedha ya Bloomberg.