Chelsea imejitayarisha kutoa ofa kwa mlinda lango mwingereza Dean Henderson, 23, ya pauni 170,000 kwa wiki ambaye sasa hivi yuko Sheffield United kwa mkopo , kujaribu kumshawishi kujiunga nao kutoka Manchester United. (Manchester Evening News)

Morally correct for Man Utd to honour Henderson loan' – Wilder ...

Henderson atatafuta kwa kila namna kuondoka tena kwa mkopo labda tu apate hakikisho kutoka Manchester United kwamba atapata fursa ya kushindana na mlinda lango wa Uhispania David de Gea, 29, awe chaguo la kwanza. (Times – subscription required)

David de Gea

Mlinda lango wa Manchester United David de Gea

Chelsea pia itajitahidi kusaini mkataba na mlinda lango wa Barcelona na Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 28, na iko tayari kutoa ofa kwa mlinda lango wa kimataifa Kepa Arrizabalaga, 25, kama sehemu ya makubaliano yoyote yale. (Mundo Deportivo, via Mail)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika kwamba mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Independent)Pierre-Emerick Aubameyang

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika kwamba Pierre-Emerick Aubameyang atasaisini mkataba mpya

Everton ina nia ya kumsajili kiungo wa kati raia wa Denmark mchezaji wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg, 24, lakini ameiarifu timu ya Toffees kwamba angependelea zaidi kujiunga na Tottenham. (Liverpool Echo)

Mlinda lango wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 27, ambaye yuko kwa mkopo Real Madrid, huenda akawa njiani kuelekea klabu ya Uingereza baada ya mchezaji huyo raia wa Ufaransa kununua nyumba ya familia yake mjini London. (Marca)Mlinda lango wa Paris St-Germain Alphonse Areola

Mlinda lango wa Paris St-Germain Alphonse Areola yuko kwa mkopo Real Madrid

Kocha wa Newcastle United Steve Bruce ataendelea na kazi yake ikiwa Henry Mauriss, mpinzani wa Saudi Arabia ambayo pia inataka kuinunua klabu hiyo, atanunua klabu ya Magpies. (Telegraph – subscription required)

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani amesema “ataangalia suala la kumleta mshambuliaji wa Uruguay, 33, Edinson Cavani katika klabu hiyo baada ya kupandishwa daraja na kuingia katika Ligi ya Premier. Cavani aliondoka Paris St-Germain msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika. (Sky Sports Italia, via Football Italia)Edinson Cavani

Leeds United inamsaka mshambuliaji wa Uruguay, 33, Edinson Cavani

Winga raia wa Austria wa Magpies ambaye yuko kwa mkopo Valentino Lazaro, 24, anafikiria mara mbili kuhusu kuondoka Inter Milan kabisa kwasababu ya kutopangwa kushiriki kweye mechi na St James’ Park. (Chronicle)

West Ham itahitajika kubadilisha mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati raia wa Czech Republic Tomas Soucek, 25, kutoka Slavia Prague hadi kuwa wa kudumu kwa pauni milioni 18.9 baada ya kuthibitishwa kwamba itaendelea kushiriki kwenye Ligi ya Premier. (Telegraph – subscription required)

The post David de Gea mwiba mkali kwa Dean Henderson, Chelsea wamkaribisha  appeared first on Bongo5.com.