Staa wa muziki nchini Diamond Platnumz ambaye pia ni Balozi wa kampuni ya Michezo ya kubashiri ya Parimatch, Jumanne hii amekabidhi kompyuta maalum zitakazotumika kwaajili ya mafunzo ili kuweza kuendana na kasi ya teknolojia na kujiandaa vyema na mahitaji ya soko la ajira au kujiajiri kwa watoto yatima kutoka kituo cha Huruma Islamic na Amani Foundation.

Pia Diamond amekabidhi runinga, jenereta na vyakula kwa vituo hivyo viwili, Huruma Islamic na Amani Foundation.

Mara baada ya kutoa msaada huo, Akizungumza na Waandishi wa Habari, Diamond Platnumz amesema kuwa anapenda kufanya kazi na kampuni zinazothamini watu kwenye jamii, sio kuangalia biashara tu.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana amesema kwamba wanapenda umma utambue kuwa kampuni yao imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii hususani katika nyanja za elimu, michezo, na mazingira.