Zitto amkaribisha rasmi Membe ACTMwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake hakijapokea barua wala ujumbe wa simu toka kwa aliyekuwa mwanachama wa CCM Bernad Membe juu ya kutaka kuhamia kwenye chama hicho.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum na kituo cha televisheni mtandao cha Watetezi TV Maalim Seif amesema hata Membr mwenyewe bado hajatoa kauli yoyote hivyo watu wasubiri.

“Mimi kama Mwenyekiti wa chama sijapokea barua ya Bernad Membe au kunipigia simu kama anakuja kwenye chama chetu cha ACT Wazalendo na pia Bernad Membe hajatoa kauli kama anakuja” amesema Maalim Seif

Ikumbukwe kuwa kwa siku kadhaa zilizopita waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje amenukuliwa akisema kuwa yupo tayari kugombea kwenye nafasi ya urais ili kupambana na rais John Magufuli iwapo tu ataomba na vyama vya upinzani au chama chake cha CCM kitamsafisha na kumpa ridhaa ya kuwa mgombea kwenye uchaguzi ujoa mapema mwezi Oktoba.