SASA ni dhahiri kuwa Bernard Kamilius Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa nchini Tanzania, yuko mbioni kujiunga na ACT – Wazalendo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wandamizi wa ACT- Wazalendo zinasema, majadiliano kati ya mwanasiasa huyo na viongozi hao juu ya kujiunga kwake na chama hicho, tayari yamekamilika