Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametangaza kusitishwa kwa shughuli za kumpokea mtiania ya kugombea wa urais wa chama hicho  Bernard Membe mkoani Lindi kutoka na kifo cha Rais msaafu Benjamin Mkapa.

Zitto ametangaza maamuzi hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter leo Julai 25, 2020 na kusema chama hicho kinaendelea kutoa pole kwa familia ya Mkapa na taifa kwa ujumla.

“Tumeahirisha shughuli yetu ya kisiasa Leo ya Wananchi wa Lindi kumkaribisha Bernard Membe nyumbani ili kupisha shughuli za maombolezo ya Rais Mstaafu Benjamin W Mkapa. Tunaendelea kuwapa pole Watanzania na Famiia ya Rais Mkapa kwa msiba mzito huu. Maisha ya Mkapa kiuongozi ni Mafunzo” ameandika Zitto.

Rais Mkapa alifariki usiku wa kuamkia Julai 24,2020 akiwa hospitali jijini Dar es salaam alikikuwa akipatiwa matibabu na anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano julai 29,2020 Mkoani Mtwara.