Rais Magufuli amemteua Kamanda wa Kikosi cha Polisi TAZARA, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega akichukua nafasi ya Godfrey William Ngupula

Aliyekuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Solomon Isack Shati ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang akichukua nafasi ya Bryceson Paul Kibasa

Aidha, Waziri wa Utumishi, Kept (Mst) George Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais Magufuli amemteua Omary Mwanga kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea akichukua nafasi ya Husna Juma Sekiboko

Pia, Waziri Mkuchika amemteua aliyekuwa Afisa Tarafa Wilayani Mbulu, Saitoti Zelothe Stephen kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya akichukua nafasi ya Hassan M. Mkwawa