Mwanasheria maarufu Nchini Tanzania "Albert Msando" nae ametoa yake kuhusu kipigo alichokipata msanii wa Bongofleva Shilole
Albert Msando amefunguka kisheria zaidi

''Police Tanzania nimemsikia anayeitwa Uchebe amenukuliwa kwamba hizi picha ni za zamani. Hivyo kimsingi amekubali kwamba alimpiga Shilole ila zamani. MIMI NIMESIKILIZA NA KUSOMA ALICHOSEMA KAMA MNAHITAJI SHAHIDI. Kosa la jinai halina muda. Hata kama lilifanyika miaka ya 1980! Kama lilikuwa ni kosa kisheria basi aliyetenda lazima adhabu inamuhusu. Nitashangaa kama ‘upelelezi bado unaendelea’ mpaka ikifika mwezi wa nane. Ni vyema muda akitoka jela akute kiberiti kinauzwa elfu 15 na box spanner inauzwa kama laki 6 hivi. Tuone gereji atakuwa na spanner ngapi na ghetto atawasha jiko la mchina na nini.