MSANII wa Vichekesho, Idriss Sultan (27) na wenzake wawili wamesomewa upya mashitaka ya kuchapisha maudhui bila leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia na kumkamata tena.

Mbali na Sultan ambaye ni Mkazi wa Mbezi Beach washitakiwa wengine ni Dokta Ulimwengu (28) Mkazi wa Msasani na Isihaka Mwinyimvua (22) Msanii na Mkazi wa Gongo la Mboto.

 
Washitakiwa hao awali walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambae awali alifuta kesi hiyo na washtakiwa walikamatwa na kusomewa upya mashtaka hayo.