Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa Julai 28, 2020, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu atahudhuria shughuli za utoaji wa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Benjamin william Mkapa, katika Uwanja wa Uhuru. 


Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 26, 2020, na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene, na kwamba ratiba ya shughuli zingine itatolewa. 


Aidha chama hicho kimesisitiza kwa wale ambao wataenda kumpokea Lissu hapo kesho Julai 27, wafanye hivyo kwa utulivu, amani na upendo mkubwa