Breaking News: Rais magufuli atangaza rasmi uwanja Taifa uitwe Mkapa Stadium
Rais John Magufuli ametangaza rasmi Uwanja wa Taifa sasa utaitwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa (Benjamin William Mkapa Stadium) kwa kuenzi mchango wake kwenye kuendeleza michezo.
“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo,kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’, Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwakuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium”-JPM