Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, wametangaza kuchukua fomu leo ya kugombea katika majimbo yao waliyokuwa wanayaongoza.

Lema amesema leo majina ya saa tano atakwenda kuchukua fomu ya kuendelea kuwa mbunge wa Arusha Mjini 2020 hadi 2025.