Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally amesema chama chake hakitishwi na kitendo cha mwanasiasa Maalim Seif Hamad kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kwa mara ya tano kwani ni chama chake kipya (ACT-Wazalendo) hakina mtandao.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha Utv  Dkt Bashiru amesema Maalim Seif ni mwanasiasa mzoefu wa kushindwa kwenye uchaguzi hivyo CCM haitishwi na kugombea kwake.

“Maalim Seif yeye ni mzoefu wa kushindwa lakini zamu hii ni mgeni katika chama chake kwa hiyo leo hii tunashindana na mzoefu wa kushindwa na mgeni katika chama ambacho hakina mtandao” amesema Dkt Bashiru.

Ikumbukwe kuwa Maalim Seif atagombea urais kwa mara ya sita kwa upande wa Zanzibar na mara zote alizogombea ameshindwa kunyakua kiti hicho