Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, amekubali kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo na kwamba huo ni wakati muafaka kwake wa kushiriki mazungumzo na Vyama vingine ili waweze kusimamisha mgombea mmoja.

Kuupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, “Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama CHADEMA ili tusimamishe ‘Kisiki cha Mpingo’ kimoja!”.
Jana wakati akizungumza alisema haya “Mimi nimefukuzwa tena kwa aibu na kutukanwa na vijana ambao ningeweza kuwazaa, na sikutenda kosa lolote hata mbele ya Mungu, kosa nililofanya ni la kugombea Urais 2015, milango imefungwa na kufunguliwa na ACT na nikakaribishwa chumbani”.