Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (kushoto) akizungumza katika kikao maalum na uongozi wa Kampuni ya Kagera Sugar Limited, wakati wa ziara yao ya kutembelea Kiwanda cha Sukari cha Kagera, kilichopo Misenyi Mkoani Kagera mwishoni wa wiki. Benki ya CRDB ni moja ya Mabenki yaliyofanikisha Kujengwa kwa Kiwanda cha Sukari cha Kagera kuanzia hatua za awali kabisa. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifafanua jambo katika kikao maalum kati ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na uongozi wa Kampuni ya Kagera Suger, wakati wa ziara yao ya kutembelea Kiwanda cha Sukari cha Kagera, kilichopo Misenyi, Mkoani Kagera mwishoni wa wiki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kagera Sugar Limited, Ashwin Rana (aliyesimama kushoto) akitoa taarifa ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, wakati walipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Misenyi, Mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kagera Sugar Limited, Seif Ally Seif (kushoto) akifafanua jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, wakati walipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kagera.