Wachunguzi wa Iran wamesema betri ya kombora ambayo haikukaa vizuri mahala pake na kutokuelewana vyema kati ya wanajeshi na makamanda wao ndio sababu ya walinzi hao wa mapinduzi kuiangusha ndege ya abiria ya Ukraine mnamo mwezi Januari ambapo watu 176 waliuawa.

Ripoti iliyotolewa na shirika la usafiri wa anga la Iran, imetolewa miezi kadhaa baada ya kuanguka kwa ndege hiyo mnamo Januari 8 karibu na Tehran ambayo kwa siku kadhaa, serikali ilikanusha kuhusika.

Bad communication blamed for Ukrainian jet downing in Iran

Tukio hilo lilitokea usiku ambao Iran ilifanya shambulizi la kombora lililolenga wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kwa kujibu shambulizi la ndege isiyoendeshwa na rubani ya Marekani lililosababisha mauaji ya jenerali wa jeshi la mapinduzi Qassem Soleimani nchini Baghdad.

Ripoti hiyo ilijumuisha mfululizo wa nyakati ambazo shambulizi hilo dhidi ya ndege hiyo ya Ukraine nambari 752 lingeepushwa.

The post Betri yatajwa kuwa chanzo cha Iran kuilipua ndege ya Ukraine  appeared first on Bongo5.com.