Wakati Tanzania ikiendelea na mombolezo kufuatia kumpoteza aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania katika Awamu ya Nne, Bernard Membe amesema alikuwa Kiongozi wa dunia.

Membe aliyasema hayo jana mkoani Lindi, muda mchache baada ya kuahirisha Kikao cha Chama Cha ACT Wazalendo kilichokuwa kiketi mjini humo sambamba na kukutana na viongozi mbalimbali wa Chama ngazi za kata.

Alisema, Mkapa alikuwa kinara katika kusaidia bara la Afrika kuweza kutatua migogoro bila kichoka hatua ambayo imeacha pigo kubwa.

“Kwanza nichukue nafasi hii kwa niaba ya familia na Wana-ACT Wazalendo kutoa salamu kutoa pole zetu za dhati kwa msiba mzito ambao umetukuta.

” Mzee Mkapa ambaye ni Baba yetu na rais mstaafu alikuwa kiongozi siyo wa Tanzania tu bali alikuwa kiongozi wa dunia, amesuluhisha migogoro mingi, nimepokea salamu kutoka kwa Waziri wa Namibia akitoa salamu zake.

“Tutamkumbuka kwa kuwa kiongozi ambaye alitumia wakati wake mwingi kuisaidia jamii ya Tanzania, alikuwa miongoni mwa marais wazuri wa Tanzania, kifo chake kimetuletea majonzi watu wote,” alisema Membe.

Alisema yeye kama Mwana-diplomasia atamkumbuka, Mzee Mkapa kwa elimu yake, ushauri wake, maagizo yake na mafundisho yake juu ya diplomasia ya kweli, diplomasia ya kisiasa na diplomasia ya uchumi ambayo alikuwa anaisimamia.

“Nchi kama Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Burundi, Rwanda, Kenya, Sudani na Congo Mzee Mkapa ameshiriki katika utatuzi wa migogoro mbalimbali tangu aache nafasi yake ya urais mwaka 2005.

“Nina hakika baada ya kifo hiko dunia itamkumbuka kama kiongozi mahshuri barani Afrika na duniani kwa ujumla kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali iliyokuwa ikiikabili Afrika bila kuchoka kwa muda wote alipotakiwa kufanya hivyo,” alisema Membe.

Aidha, Membe aliongeza kuwa ni pigo kuona kiongozi huyo akiondoka katika wakati ambao Tanzania inaelekea katika uchaguzi Mkuu Oktoba 28, Mwaka huu.

“Katika kipindi cha Uchaguzi kama hiki ji bahati mbaya kuona kwamba tunampoteza mtu ambaye alikuwa anahimili mambo mengi ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na ushiriki wake na ushauri katika masula ya uchaguzi.

The post Bernard Membe: Mkapa alikuwa Kiongozi wa dunia sio Tanzania tu (+Video) appeared first on Bongo5.com.